Ni mchezo wa ufunguzi ulioshuhudia Simba ikitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya mabingwa wa Afrika, Al Ahly kwenye Dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Magoli ya Simba yamefungwa na Kibu Denis dakika ya 53, na Sadio Kanoute dakika ya 59 huku magoli ya Al Ahly yakifungwa na Reda Slim (45'+1) na Mahamoud Karahba dakika ya 63.