Tanzania Prisons imekubali kichapo cha mabao 2-1 ikiwa nyumbani Sokoine Stadium Mbeya kutoka kwa Mashujaa FC, ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu ya NBC, raundi ya 28.
Magoli ya Mashujaa yamefungwa na David Ulomi dakika ya 14 na Shaban Mgandila kwa penati dakika ya 20.
Prisons pia walipata pigo dakika ya 40 baada ya nahodha wao Jumanne Elifadhili kutolewa kwa kadi nyekundu.