Mashujaa FC ya Kigoma imepanda daraja kucheza ligi kuu ya NBC msimu ujao kwa kuichapa na kuishusha daraja Mbeya City kwa jumla ya magoli 4-1 baada ya mechi mbili.
,Katika mchezo huu wa marudiano uliopigwa leo Dimba la Sokoine, Mbeya, Mashujaa imeondoka na ushindi wa bao 1-0 dakika ya 87 likifungwa na John Budeba na mchezo wa mkando wa kwanza, Mashujaa ilishinda mabao 3-1 mjini Kigoma.
Katika tukio hili pia, kocha wa magolikipa wa Mashujaa amekula kadi nyekundu kwa kosa la kumpiga kwa makusudi kocha wa Mbeya City, Abdallah Mubiru,