Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu Bungeni leo, amesema kuwa Rais Magufuli alikuwa sahihi kwa mujibu wa sharia kuipandisha hadi Manispaa ya Dodoma kuwa jiji.
Majaliwa alikuwa akijibu swali la mbunge Viti Maalum kutoka mkoa wa Dodoma Felister Bulla huku akiweka wazi vigezo ambavyo vinaifanya Dodoma itoshe kuwa jiji.
Majaliwa pia ameeleza kuhusu mchakato wa kisheria wa kuitambua rasmi Dodopma kama jiji.