Baadhi ya abiria miongoni mwa wasafiri zaidi ya 800 waliokuwa wakitumia usafiri wa treni wameutupia lawama uongozi wa shirika la reli (TRC) kwa kuachwa njiani kwa zaidi ya saa 10 bila huduma muhimu baada ya treni waliyokuwa wakisafiria kukwama njiani kutokana na kuziba kwa reli.