Alasili ya Julai 17 2024 kumetokea hali ya Taharuki katika Pwani ya Kijiji cha Naumbu Wilaya na Mkoa wa Mtwara baada ya kutokea vitu vya ajabu Baharini kama Upepo ulioambatana na Moto na ulipofika Nchikavu vitu hivyo vilimvamia Mama mmoja aitwae Bi. Rukia Muwanya mkazi wa Kijiji hicho ambae alikuwa amembeba Mtoto wake.
Mama huyo alikimbilia kwenye nyumba yake ambapo baadae nyumba hiyo iliezuliwa Paa lake na kutupwa pembezoni mwa Bahari ya hindi. Hata hivyo Vitu hivyo pia vilivunja Mtumbwi wa Baba mwenye nyumba hiyo Ndugu Fadhili Ismaili na kuvuruga Choo cha Makuti cha nyumba hiyo.
SUBCRIBE YOUTUBE CHANNEL YA FAIDA ONLINE TV ILI KUPATA HABARI ZETU