TAHARUKI !! WATOTO 17 WAKUTWA KWENYE KONTENA MTWARA | WAZAZI WACHARUKA | KAMANDA ATHIBITISHA

Опубликовано: 22 Июнь 2025
на канале: Faida Online TV
29,626
166

Hivi karibuni kumekuwa kukiripotiwa matukio mbalimbali ya upotevu wa Watoto Nchini Tanzania hasa katika Mkoa wa Dar es salaam, hali inayowapa wasiwasi Wazazi pindi Watoto wao wanapokuwa shuleni au hata wakiwa Mtaani wakicheza.

Lakini katika hali isiyo ya kawaida Mlinzi anaefanya kazi ya kulinda eneo maarufu kama (Kwa Father Liumbo) Mtaa wa Mbae Mashariki kata ya Ufukoni Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara amewakamata Watoto 17 wa Shule ya msingi Muungano na kuwafungia kwenye Kontena baada ya kuwakuta Watoto hao wakiangusha Embe mbichi maarufu kama NDOLO katika miembe iliyopo kwenye eneo hilo.

Faida Online tv tumekuandalia taarifa hii.