Mtoto wa kike aitwae Muzdati Hamisi Mnaukuta mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi 9 aliyedaiwa kupotea siku ya Aprili 30, 2025, ameonekana siku ya Mei 02, 2025 akiwa mzima porini huku mwili wake wote ukiwa na siafu wakati huo imani za kishirikina zikihusishwa na tukio hilo.
Kwa upande wake Sheda Sefu Ulaya ambae ni ndugu wa Familia hiyo ameiambia Faida Online TV baada ya kufika Kijijini hapo kuwa, walipoona harakati za kumtafuta Mtoto zimegonga Mwamba, wakaamua kumtafuta Mtaalam (Mganga wa kienyeji) ambae alifanya tiba zake na siku moja baadae Mtoto huyo alionekana.
Majirani na Mashuhuda wa tukio hilo wamefurahia kuonekana kwa Mtoto huyo huku wakimsikitikia kwa mateso aliyopitia Porini kwa kipindi hicho cha siku mbili hasa ukilinganisha na umri wake.
Nae Mwenyekiti wa Kijiji hicho cha Madangwa Ndg. Salumu Hassani Kuku, amesema alitoa taarifa hiyo Polisi Mkoani Lindi, na Polisi hao wakatuma salamu kwa Ndugu wa Mtoto aliyepotea kuwa anatakiwa aonekane haraka na kweli siku moja mbele Mtoto akaonekana,
Mpaka tunakupatia taarifa hii Mtoto bado yupo katika Hospitali ya Mnazi mmoja Lindi, kwa uchumgizi zaidi wa kidaktari.
SUBSCRIBE YOUTUBE CHANNEL YA FAIDA ONLINE TV ILI KUPATA HABARI ZETU.