WATATU WAFARIKI KWA AJALI YA BODABODA NANGURUWE MTWARA | MMOJA AACHA MKE MJAMZITO

Опубликовано: 22 Июнь 2025
на канале: Faida Online TV
18,965
86

Vijana Watatu wakazi wa Kata ya Nanguruwe Halmashauri ya wilaya na mkoa wa Mtwara, ambapo Wawili kutoka Kijiji cha Nanguruwe na mmoja kutoka Namahyakata barabarani wamefariki Dunia baada ya kugongwa na Gari wakiwa kwenye Bodaboda katika eneo linalojengwa Kongani la viwanga vya ubanguaji wa Korosho kwenye Kijiji cha Maranje wakielekea Kijiji cha Mbembaleo kufunga Vifaa vya Mziki.

Tukio hilo limetokea jana Novemba 08 2024 majira ya saa 12 jioni huku Marehemu hao ikiwa ni pamoja na Jamali Nyati, Hamisi Mchina na Saidi Namkava ambapo miili miwili ililazimika kuzikwa jana usiku kutokana na kuharibika kwake, na Mwili mmoja umezikwa leo Novemba 9 2024 saa 4:00 asubuhi hapohapo Nanguruwe.

Akiongea na Faida Online tv Dtk. Shamila Athumani ambe ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Mtwara iliyopo Nanguruwe amekili kupokea miili hiyo mitatu ambapo amesema walikuwa wamefariki papo hapo katika eneo la tukio.

Faida Online tv tutazidi kufuatilia kujua kama Dereva aliyesababisha ajali amekamatwa au laa.

SUBSCRIBE YOUTUBE CHANNEL YA FAIDA ONLINE TV ILI KUPATA HABARI ZETU