MAAJABU: UA LAOTA JUU YA KABURI SIKU MOJA BAADA YA MAZISHI MTWARA.

Опубликовано: 22 Июнь 2025
на канале: Faida Online TV
54,138
420

Wananchi wa Kijiji cha Namgogoli Kata ya Naumbu wilaya na Mkoa wa Mtwara, wamekutwa na butwaa baada ya kushuhudia Ua likiwa limeota juu ya Kaburi la Ndugu Moammed Jumaa, siku moja baada ya kuzikwa na likachanua hali iliyoleta Mshangao kwa kuwa sio jambo la kawaida.

Akizungumza na Faida Online tv leo Desemba 6, 2024 Kijijini hapo, Mpwa wa Marehemu aitwae Ally Ahmadi Mkoto amesema Marehemu amezikwa siku ya Desema 4 2024 saa 7 mchana, na mpaka kufikia jioni ya siku hiyo juu ya Kaburi hilo hapakuwa na chochote lakini walipoenda kuzuru Kaburi hilo asubuhi wakakuta Ua kubwa likiwa limeota.

Ndugu Mkoto ameongeza kuwa Marehemu enzi za uhai wake alikuwa Mcha Mungu ambae aliwahi pia kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Imamu wa Msikiti wa Kijiji hicho na baadae kuwa Mzee wa Msikiti mpaka anakutwa na umauti, hivyo Familia wanaona kuwa ni dalili njema kwa Mzee wao huko aliko.

Kwa upange wake Ndg. Salumu Mohammed bin Jumaa ambe ni Mtoo wa Marehemu anayeishi Songea, amesema Mzee wake alikuwa Mtu wa ibada wakati wote, hata Watoto wake aliwalea katika misingi ya Dini, Lakini pia alitumia muda wake mwingi kuhimiza Watu kufanya ibada.

Bi. Asha Mohammed Jumaa, ni Mtoto wa marehemu ambae tumemkuta Kijijini hapo ambae nae hakwenda tofauti na wengine, amesema hiyo ni alama njema kwa Mzee wao huku akiongeza kuwa Mzee huyo alikuwa akiwasaidia hata Watu asiowajua enzi ya uhai wake iwe Chakula hata Malazi.
Kwa pamoja tunasema Inna lillah wainna ilaihi rajiun, Mungu aiweke roho ya Marehemu mahala pema peponi aamin.

SUBSCRIBE YOUTUBE CHANNEL YA FAIDA ONLINE TV ILI KUPATA HABARI ZETU