Wananchi wa Kijiji cha Mnyundo, kata ya Ndumbwe Halmashauri ya Wilaya na Mkoa wa Mtwara, wamesema chanzo chao cha Maji wanachokitumia kwa shughuli mbalimbali kama vile kunywa, Kuoga, Kufulia na hata kumwagilia bustani wakiwasha moto juu ya Maji hayo unawaka na hauwezi kuzimika hadi uzimwe kwa Mchanga au Majani.
Wakiongea na Faida Online tv (WATU WA FIELD) baada ya kutembelea Kijijini hapo Wananchi hao wamesema kuwa kutokana na hali hiyo wanahisi kuwa Mahali hapo pana Gesi ingawa hawana uhakika maana kuna mda pana asili ya kuwa na Mvuke hasa kipindi cha Jua kali.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji hicho cha Mnyundo Ndg. Rashidi Mussa, amethibitisha uwepo wa hali hiyo huku akiongeza kuwa wametoa taarifa kwa Mamlaka yanayohusiana na mambo ya Gesi ikiwemo TPDC ambao walifika Kijijini hapo na kujionea hali hiyo kisha kuchukua kiasi cha maji kwa ajili ya kwenda kuyapima wajue nini kipo ndani yake.
SUBSCRIBE YOUTUBE CHANNEL YA FAIDA ONLINE TV ILI KUPATA HABARI ZETU.