MWANAMKE AJINYONGA BAADA YA KUFUMANIWA MTWARA| AACHA WATOTO WAWILI.

Опубликовано: 22 Июнь 2025
на канале: Faida Online TV
47,609
197

Mtu mmoja aliefahamika kwa jina la Raima Issa Mtalala, mwenye Umri wa miaka 24 aliyekuwa akiishi kwenye Kijiji cha Tulia Kata ya Mtiniko Halmashauri ya Mji Nanyamba mkoani Mtwara, amekutwa akiwa amefariki Dunia baada ya kujinyonga ndani ya Banda la Nyumba ya Mamaake mzazi huku chanzo kikidaiwa kuwa amefumaniwa.

Wakati akichukua hatua hiyo, Mume wake alikuwa Jijini Dar es salaam kutafuta maisha ambapo alipigiwa simu na kupewa taarifa hiyo ya kifo kilichotokea siku ya Oktoba 31 2024.