Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mussa Ally Nassoro mkazi wa Kijiji cha Mgao kata ya Naumbu Wilaya na Mkoa wa Mtwara ambae ana matatizo ya akili, inasemekana alifariki Dunia siku ya Novemba 30, 2024 na kuzikwa na wale waliojithibitishia kuwa ni ndugu yao Lakini ndani ya wiki hiyo hiyo, Mtu anaefanana na huyo alionekana Mtaani na kuongoza hadi katika Nyumba hiyo aliyokuwa akiishi ambayo ndiyo ilikuwa na msiba, na kufanya Ndugu washikwe na butwaa,
Akiongea na Faida Online tv Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara SACP Issa Suleiman amesema Watu hao wamezika Mtu ambae sio ndugu yao na wa kwao ni huyu ambae yupo hai.
SUBSCRIBE YOUTUBE CHANNEL YA FAIDA ONLINE TV ILI KUPATA HABARI ZETU