Kocha wa Yanga SC, Miguel Gamond amesema mechi yao ya Jumamosi ya NBC Premier League dhidi ya Coastal Union itakuwa ngumu kama ilivyozoeleka kwa timu hizo zinapokutana.
Golikipa wa timu hiyo Abutwaleeb Mshery naye amesema wanatamani kuona wakiibuka na ushindi kwenye mchezo huo.