ITAKUSHANGAZA YALIYOJIFICHA UNUNIO SEHEMU TULIVU, MATUKIO YA KUTISHA, MWENYEKITI AFUNGUKA

Опубликовано: 13 Ноябрь 2024
на канале: Mwananchi Digital
38,192
170

Ununio ni moja ya maeneo yaliyopo wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, likiwa kaskazini mwa Jiji jirani na Bahari ya Hindi.

Eneo hili lililo jirani na Mbezi Beach na Tegeta linajulikana kwa kuwa na fukwe nzuri na mandhari ya utulivu, likikua kwa kasi katika maendeleo ya miundombinu ya makazi.

Ununio ikiwa moja ya mitaa katika Kata ya Kunduchi ina wakazi 7,469 kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa huo, Mwinyijuma Shehe.

Hata hivyo, kama maeneo mengine ya pembezoni mwa jiji, Ununio bado lina maeneo ambayo hayajapimwa vizuri, huku kukiwa na nyumba zilizokamilika ujenzi lakini hazikaliwi na watu, zingine zikiwa hazijakamilika ujenzi.