KATIBU MKUU CHADEMA MNYIKA ADAI KUITWA POLISI, RPC AKANA TAARIFA, WAKILI AHUSISHA NA UTEKAJI

Опубликовано: 11 Ноябрь 2024
на канале: Mwananchi Digital
30,408
92

Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika ametakiwa kuripoti Kituo cha Polisi Oysterbay Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano, Wakili wa chama hicho amethibitisha.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Septemba 12, 2024 Wakili wa Chadema, Hekima Mwasipu amesema kiongozi huyo ameitwa na Ofisa Upelelezi wa Mkoa (RCO) wa kipolisi wa Kinondoni, japo hawakuambiwa anaitiwa nini.

“Ni sahihi kwamba Mnyika ameitwa. Tuliletewa taarifa kwamba anaitwa, lakini kwa sasa yupo mkoani Tabora. Nitampeleka kesho (Septemba 13, 2024),” amesema.