Watu watano akiwamo bibi wa miaka 70, Felista Mwanri na mwanawe Richard Mwanri (47) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakabiliwa na shtaka la kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi zenye uzito wa zaidi ya tani moja.
Washtakiwa wengine ni Athuman Mohamed, maarufu Makame (58) mkazi wa Tanga, Juma Chappa (36), mkazi wa Kiwalani na Omary Mohamed (32) ambaye ni dereva na Mkazi wa Buza, Dar es Salaam.