KULIKUWA NA MIGOGORO YA KANISA ASKOFU ALITUSAIDIA, ALITHAMINI WATU KIFO CHAKE KIMETUGUSA

Опубликовано: 11 Ноябрь 2024
на канале: Mwananchi Digital
2,730
9

Nguzo imeanguka, hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya wachungaji wa Dayosisi ya Mwanga ya Kanisa la Kiinjili la kilutheri Tanzania(KKKT)kusimulia namna Askofu Chediel Sendoro alivyoweza kuwaunganisha wanadayosisi hiyo na kuondoa makundi.

Askofu Sendoro alifariki Septemba 9,2024 kwa ajali ya gari iliyotokea katika eneo la Kisangiro, Wilaya ya Mwanga, Mkoani Kilimanjaro saa 1:30 usiku, baada ya gari alilokuwa akiendesha aina ya Toyota Prado, akitokea Kileo kuelekea nyumbani Mwanga, kugongana uso kwa uso na lori.

Akizungumza Mchungaji Msifuni Luka ambaye ni mchungaji kiongozi wa usharika wa Mchali Dayosisi ya Mwanga, amesema wamempoteza kiongozi ambaye alitumika kwa nguvu na uaminifu na kuhakikisha anawaunganisha watu na kuondoa makundi.

Mchungaji wa Usharika wa Mruma, amedema Askofu Sendoro alikuwa kiungo kikubwa katika Dayosisi hiyo na aliweza kuwaunganisha watu wote.

Mthiolojia Silvanus Msuya, amesimulia namna Askofu Sendoro alivyomchukua kutoka Dar es salaam na kumleta Mwanga kusomea uchungaji.

Msuya ambaye amemaliza Masomo ya uchungaji katika chuo kikuu cha Tumaini Makumira na anasubiri kubarikiwa, amesema Askofu Sendoro alimtoa katika namna ambayo si njema na kumpeleka katika kumtumikia Mungu.