Serikali imewapa Sh15 bilioni Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ili waweze kununua mahindi ya wakulima.
Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi Septemba 2, 2021 na waziri mkuu, Kassim Majaliwa wakati akijibu swali la mbunge wa Kwela aliyehoji Serikali ina mpango gani katika zao la mahindi katika kipindi ambacho wakulima wanaendelea kutafuta masoko.
Mbunge huyo amehoji namna Serikali ilivyojipanga ili kuziwezesha taasisi za Serikali kama NFRA ziweze kununua mahindi ya wakulima.