Front-end website development imejengwa na nguzo kuu tatu, ambazo ni HTML, CSS na Javascript. Ndani ya hii kozi, nitakufundisha fundamentals yaani misingi ya Javascript. Utakapo maliza kozi hii, utakua umemaliza hatua muhimu za mwanzo katika safari yako ya kua professional front-end developer. Kwa majina ninaitwa George Raphael Kitula, Mimi ni mtaalam wa website Pamoja na mobile application development. Nina uzoefu wa zaidi ya miaka kumi sasa katika fani hii. Lengo langu kuu ni kuifupisha safari yako ili uweze kutimiza ndoto zako za kua professional website developer katika muda mfupi zaidi, yaani web developer wa ukweli na si mbabaishaji. Je, Upo tayari? Kama jibu lako ni ndio, basi tukutane katika video inayofuata asante.