/ uwazi1
Hivi Ndivyo Ilikuwa Mara ya Mwisho Mama Kumuona Mtoto Kabla ya Kutekwa na Kuuawa
Tukio la utekaji wa watoto wawili kisha miili yao kupatikana wakiwa wamefariki na kutupwa kwenye chemba ya choo, limeacha simanzi nzito kwa wazazi wa watoto hao. Wazazi wa Maureen, mtoto ambaye naye alitekwa na kuuawa, wanasimulia jinsi tukio hilo la kikatili lilivyotokea ambapo mama mzazi wa Maureen anasimulia kwamba siku ya tukio, mwanaye alitoka nje kucheza na wenzake lakini hakurudi mpaka giza lilipoingia.
Mwanamke huyo anaendelea kusimulia mkasa mzima, jinsi walivyopokea barua kutoka kwa watekaji, wakiwataka watume fedha ili warudishiwe mtoto wao vinginevyo watarudishiwa kichwa tu.
Naye baba wa marehemu anasimulia kwa kina kila kitu kilichoendelea, jinsi walivyohangaika kumtafuta mtoto huyo mpaka walipopokea taarifa kwamba mwili wa mtoto wao pamoja na mtoto mwingine aliyetekwa, Ikram imepatikana kwenye chemba ya choo wakiwa wameuawa.
subscribe kwenye chanel yetu kwa kubofya… / uwazi1 / uwazi1 / uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOK: / globalpublis. . TWITTER: / globalhabari INSTAGRAM: / globalpubli. .